Kikois cha Simba SC kimerejea jijini Dar es salaam kikichokea mjini Marrakech-Morocco, kilipokuwa kikikabiliwa na mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydac AC.

Simba SC ilipoteza mchezo huo uliopigwa Jumamosi (Desemba 09) saa nne usiku na kujikuta ikiporomoka kutoka nafasi ya tatu hadi ya nne katika msimamo wa Kundi B.

Baada ya kurejea nchini kikosi cha Simba SC kitajiandaa na mchezo wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Ijumaa (Desemba 15) Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Baada ya mchezo huo wa Ligi Kuu, Simba SC itaanza kujiandaa na mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi B, ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad A.C.

Mchezo huo wa Mzunguuko wanne umepangwa kuchezwa Jumanne (Desemba 19), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ambapo Simba SC italazimika kusaka ushindi ili kufufua matumaini ya kufuzu Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ikitokea Kundi B.

Endapo matokeo yatakuwa tofauti na ushindi, Simba SC itakuwa imejiondoa katika mbio za kuwania nafasi ya kucheza Robo Fainali msimu huu, na itakuwa mara ya kwanza kwao, tangu msimu wa 2018-19.

Simulizi: Akili ndogo inavyoweza kuipiku akili kubwa
Mradi wa Maji Ziwa Victoria kuvinufaisha Vijiji 33