Mabingwa Watetezi wa Tanzania Bara Simba SC wanaamini Jumamosi (Desemba 11) itakua siku rasmi kwao kukaa kileleni kwa mara ya kwanza msimu huu 2021/22.
Simba SC itaikaribisha Young Africans Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam Jumamosi (Desemba 11), katika mchezo wa Mzunguuko wanane wa Ligi hiyo.
Akizungumza katika Mkutano na Waaandishi wa Habari leo Jumatano (Desemba 08), Msaidizi wa Afisa Habari wa Simba SC Ally Sharty ‘CHIKO’, amesema kikosi chao kipo katika mkakati mkali wa kujiandaa mchezo huo, na wana matumaini makubwa ya kuibuka wababe siku hiyo.
Amesema Maandalizi ya mchezo huo yalianza tangu Jumatatu (Desemba 06) mjini Lusaka-Zambia, na leo Jumatano (Desemba 08) jioni kitaendelea na mazoezi baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam jana Jumanne (Desemba 07) majira ya usiku.
“Tunaamini mchezo huu utaturudisha kwenye nafasi yetu, tumeshazoea kuwatanguliza ndugu zetu, na ndivyo ilivyo kwa msimu huu,”
“Kikosi kilianza maandalizi ya mchezo huu tangu Jumatatu (Desemba 06) kikiwa mjini Lusaka-Zambia, na leo Jumatano (Desemba 08) kitaendelea na mazoezi baada ya kuwasili nchini Jana Jumanne (Desemba 07).” amesema Sharty
Mchezo wa Mwisho dhidi ya Young Africans, Simba SC ilipoteza kwa kufungwa 1-0, bao likifungwa na Mshambuliaji kutoka nchini DR Congo Fiston Kalala Mayele.