Klabu ya Simba inapenda kuwashukuru wakazi wa Manispaa ya Mji wa Dodoma na Vitongoji vyake kwa kuja uwanjani kwa wingi siku ya Jumamosi,pale Klabu yao ilipocheza na timu ya Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri.

Kwa umati ule klabu yetu inaamini haikukosea kwenda Dodoma kufuatia mwaliko wa  chama cha mpira cha mkoa wa Dodoma(Dorefa) na wabunge wetu ambao ni washabiki wa Simba.

Pia tunawashukuru wote waliofanikisha ziara hii maalum iliyoleta tija kwa klabu na timu kwa ujumla.

Tutumie pia fursa hii kutoa pole kwa mchezaji wetu Peter Manyika jnr kwa kufiwa na babu yake, pia tumpe pole Manyika Peter snr ambae ni baba mzazi wa mchezaji wetu huyo na golokipa wa zamani wa Yanga kwa kuondokewa na baba yake mzazi.

Mwenyezi Mungu awape nguvu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa Mzee wao huyu na Mungu amrehemu marehemu.

Na katika kuelekea mechi yetu dhidi ya Ruvu Shooting. Klabu inayo furaha kuwaarifu wanachama na washabiki wake kuwa jezi rasmi za msimu wa 2016|17 teyari zipo madukani hapa jijini.

Jezi hizi zinauzwa kwenye maduka ya Simba sports Shop pale Dar Free Market mkabala na njia ya kuelekea Leaders Club,

Maduka ya UHL Sports yaliyopo Sinza kijiweni na makutano ya mitaa Jamhuri na Zanaki pale Round About ya kuelekea DTV.

Tunawaarifu bei elekezi ya Jezi ni shilingi elfu ishirini kwa pea moja ya jezi.

Pia kwa matawi yatayokuwa tayari kuuza jezi hizi kwa wanachama wake na washabiki wengine,wanaweza kuwasiliana na mimi na watapata punguzo maalum kutegemea idadi ya jezi watakazonunua.

Ni imani yetu kila mmoja atavaa jezi halisi(original)kuepuka kuingia katika kuhujumu mapato ya Klabu kupitia jezi hizi.

Imetolewa Na Haji S.Manara

Mkuu Wa Habari Simba SC

Simba Nguvu Moja

Baada Ya Kuikacha AFCON 2017, Chad Yaibukia Ufaransa
Dimitri Seluk: Man City Itapoteza Mamilioni Ya Mashabiki