Klabu ya Simba imemtema mlinzi wake wa kulia aliyesajiliwa siku za karibuni, Mcongo, Janvier Besala Bokungu baada ya kutoliridhisha benchi la Ufundi chini ya kocha mkuu, Joseph Marius Omog.

Simba imefikia maamuzi hayo na sasa nafasi yake inazibwa na Malika Ndeule ambaye rasmi amesaini Simba akitokea Mwadui FC na tayari jina lake lilishawasilishwa TFF kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano Tanzania bara.

Hata hivyo imefahamika kwamba nafasio ya Janvier Bokungu raia wa DR Congo huenda ikazibwa na Julius Ntambi wa URA ya Uganda.

Tangu awali kumekuwepo na taarifa kwamba kiwango cha Bokungu hakikuwaridhisha wengi ndani ya Simba ambapo walifikia hatua ya kumpa mkataba wa miezi sita huku wakiwa wanaendelea kutafuta mbadala wake.

Ntambi mwenye miaka 24 ndiye aliifungia URA bao la kwanza katika mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa mwezi Januari.

Simba bado wana nafasi ya kufanya marekebisho kwa wachezaji wao wa kigeni kwani dirisha la usajili kwa upande wa wachezaji hao halijafungwa.

Yusuph Manji Arejesha Matumani Kwa Wanachama
Mahrez Ategua Kitendawili, Ataja Klabu Anazozitamani