Beki kutoka Kenya Joash Onyango na Mshambuliaji Mtanzania Habib Kyombo hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Singida Fountain Gate kitakachoikabili Simba SC.

Wawili hao wanaocheza kwa Mkopo Singida Fountain Gate wakitokea Simba SC, wanabanwa na makubaliano yaliyofikiwa kimkataba baina ya pande hizo mbili.

Ikumbukwe kuwa Singida Fountain Gate itacheza na Simba SC leo Alhamis (Agosti 10) katika Nusu Fainali ya Pili ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa CCM Mkwakani jijini Tanga.

Mshindi wa mchezo huo atacheza dhidi ya Young Africans iliyotangulia Fainali baada ya kuigunga Azam FC jana Jumatano (Agosti 09), Uwanjani hapo.

Nkunku kuwa mtazamaji Chelsea
Man Utd yaingia mkenge