Msafara wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC umewasili mjini Berkane-Morocco usiku wa kuakia leo, tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane.

Simba SC itakua mgeni wa mchezo huo kesho Jumapili (Februari 27), huku ikichagizwa na hatua ya kuwa kinara wa ‘Kundi D’ kufuatia kushinda mchezo wake wa kwanza dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa 3-1, na kutoa sare ya 1-1 dhidi ya USGN ya Niger.

Kabla ya kuelekea mjini Berkane, Simba iliweka kambi ya siku tatu mjini Casablanca kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo, huku Benchi la Ufundi chini ya Kocha Mkuu Franco Pablo Martin likiwa na matumaini makubwa ya kupambana na kupata matokeo chanya.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC Mulamu Ng’ambi alitangulia mjini Berkane kwa ajili ya kuweka mipango sawa, na wakati timu ilipowasili Uwanja wa Ndege wa mji huo alifika kuipokea.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez aliuanga na Msafara wa Simba SC mjini Casablanca, baada ya kutangulia mjini humo kwa ajili ya kuweka mipango ya maandalizi sawa, kama ilivyokua kwa Mtaribu wa klabu hiyo Abbas Ally alipotangulia mjini Niaemy nchini Niger.

Simba SC inaongoza msimamo wa ‘Kundi D’ ikiwa na alama 04, ikifuatiwa na ASEC Mimosas yenye alama 03 sawa na RS Berkane, huku USGN ikiburuza mkia wa kundi hilo kwa kumiliki alama moja.

Lautaro Martinez kupigwa bei Inter Milan
Mwanachuo aaga dunia baada ya jogoo wake kusimama siku 3 mfululizo