Timu ya Tanzania Prisons imetangaza kuingia mkataba wa udhanini na kampuni ya uuzaji na usambazaji viatilifu na mbolea, Bens Agro Star uliotajwa kuwa na bonsai lukuki kuelekea mechi zao dhidi ya Simba SC na Young Africans.

Ofisa Habari wa Prisons, Jackson Mwafulango ameeleza kwamba mkataba huo wa mwaka mmoja uliosainiwa mwishoni mwa juma lililopita una thamani ya Sh milioni 150.

Aidha, Mkurugenzi wa Berns Agro, Patrick Mwalunenge amesema mbali na udhamini huo pia kuna ofa mbalimbali ikiwemo zawadi ya Sh milioni 10 kwa timu hiyo endapo itazifunga Simba SC na Young Africans huku ikitolewa Sh milioni moja kwa kila bao katika mechi ya ushindi.

Lakini pia kuongeza motisha, kwenye kila ushindi kocha wa timu hiyo, Fred Minziro atazoa kitita cha Sh 500,000 huku mwisho wa msimu mchezaji bora wa timu hiyo, atapewa zawadi ya kujengewa nyumba.

Lakini pia kuna suala la usafiri wa basi la kisasa ambalo tutalishughulikia siku za usoni, pamoja na mambo mengine ikiwemo kukarabati hosteli za wachezaji, hivyo niwaombe benchi la ufundi na wachezaji wote kupambana zaidi,” amesema Mwalunenge

Kwenye Ligi Kuu Bara mpaka sasa Prisons inashika nafasi ya 14 baada ya mechi saba ikiwa imeshinda mara moja, sare tatu na kufungwa mara tatu.

Skudu afunguka ishu ya kusugua benchi
Arsene Wenger aichambua Man Utd