Mabingwa wa soka Tanzania Bara Wekundu Wa msimbazi Simba leo jioni watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon katika uwanja wa Chamazi Complex, jijini Dar es salaam.

Simba watautumia mchezo huo kama sehemu ya kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Gwambina FC, ambao utapigwa Jumamosi, Septemba 26 Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja jioni.

African Lyon nao watautumia mchezo huo kama sehemu ya kujiandaa na Mshike Mshike wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania abara ambao utaanza baadae mwaka huu.

Kupitia katika ukurasa wa Instagram ya Simba umeeleza: “Kwa burudani ya jana (Juzi jumapili) ilivyokuwa nzuri tumeona ni vyema na kesho (Leo) wanasimba tuipate tena, Simba wawili tunakutana, sisi wakubwa (Simba SC) na Simba wadogo (African Lyon)” imeeleza taarifa hiyo.

Membe, Maalim Seif wapishana kauli
Selfie za kifo: Aanguka nje ya dirisha la gari likiwa kasi akijirekodi video

Comments

comments