Klabu ya Simba imetoa msimamo wake kuhusiana na sarakasi za klabu ya Azam kuruhusiwa kushiriki mashindano maalum ya kimataifa nchini Zambia.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kuwa timu yao haitakubali kucheza mechi ya raundi ya ishirini ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga endapo timu zote hazitakuwa zimechezwa idadi ya mechi sawa.

” Msimamo wetu kama Simba, tutaendelea na ligi lakini tutaiandikia TFF kuwaambia kuwa ikifika raundi ya 20 kusiwe na kiporo chochote”

“Hatutafanya jambo la kihuni la kujialika katika mashindano ya bonanza. Tutacheza ligi kwa tahadhari hio, hatutakubali mechi za viporo. ”

Manara amesema TFF wanevunja kanuni zao wenyewe kwa kuwaruhusu Azam kushiriki mashindano yasiyo rasmi nchini Zambia huku ligi ikiendelea.

” Msimam wetu kama Simba tunaamini TFF wamevunja kanuni zao wenyewe kwa kuwaruhusu Azam kushiriki bonanza”

” Kanuni ziko wazi, zinasema ili timu ihiarishwe mechi zao za ligi inatakiwa iwe inakwenda kushiriki mashindano rasmi ya kimataifa. ”

Breaking News: Vurugu zaibuka bungeni jioni hii
Nape: TBC haitarusha 'Live' Bunge kuanzia Leo ili Kubana Matumizi