Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa anaheshimu ubora wa Nkana FC na ndio maana amefanya maandalizi makubwa kuelekea mchezo huo kwa kutambua aina ya timu anayokwenda kucheza nayo.

Ameyasema hayo mjini Kitwe nchini Zambia alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mchezo huo ni muhimu kwa kila timu inaufanya uwe na asilimia 50 kwa 50 hivyo ni muhimu kuwa makini.

”Ninafahamu Nkana ni timu nzuri lakini na sisi ni timu bora na tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo yakayotubeba kwenye mchezo wa pili jijini Dar es salaam”, amesema Aussems.

Kwa upande wa mchezaji, Haruna Niyonzima ambaye ameongea kwa niaba ya nahodha John Bocco, amesema wao kama wachezaji wameshapokea kile walichofundishwa na mwalimu na wameahidi kutekeleza uwanjani.

Hata hivyo, mchezo huo wa kwanza katika raundi ya kwanza ya klabu bingwa barani Afrika, utachezwa kesho Jumamosi kuanzia saa 10:00 jioni.

 

Kama bado nina nguvu, sitarajii kung'oka madarakani- Museveni
Marekani yazishtukia China na Urusi kuhusu Afrika