Matawi ya klabu ya Simba, yamekutana jijini Dar es Salaam leo na kupanga mikakati ya kuimaliza Yanga katika mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Jumamosi.
Kikao hicho kimeongozwa na Ustaadhi  Masoud ambaye ni mwenyekiti wa matawi ya Simba.
“Kweli tumekutana, lengo ni kuhakikisha tunachukua ubingwa na hili linawezekana. Kupanga hilo, kikubwa ni kuanza na kuifunga Yanga.
“Ili tubebe ubingwa, tukiwafunga Yanga, basi tutaendelea kufanya hivyo kwa wote walio mbele yetu,” alisema.
Ustaadhi alisema si kazi rahisi kuifunga Yanga au kushinda mechi nyingine mfululizo, ndiyo maana wanahitaji ushirikiano na kuwa pamoja.
Simba na Yanga zinakutana Jumamosi katika mechi yao ya mzunguko wa pili huku kila moja ikitaka kushinda.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Simba ililala kwa mabao 2-0, hivyo inataka kulipa kisasi na pia kuendelea kubaki kileleni mwa Ligi Kuu Bara.

chanzo: Saleh Jembe

P – Square yasambaratika? Peter na Paul wapeana makavu
Mzazi Wa Cavani Ataka Mwanae Achezee Timu Hizi