Mshambulizi raia wa Senegal, Pape N’daw amekamilisha usajili wa Simba SC kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara na michuano ya kombe la FA.

Simba inayotarajia kuanza msimu wa 2015/16 kwa kucheza na African Sports ya Tanga mwishoni mwa wiki ijayo imekamilisha usajili wa nafasi zote 7 za wachezaji wa kigeni.

Simba imewasaini jumla ya wachezaji 16 wapya huku idara ya ushambulizi akibaki kijana Ibrahim Ajib pekee kutoka katika kikosi cha msimu uliopita.

Wachezaji raia wa Uganda, Hamis Kizza, Juuko Mursheed, Simon Sserunkuma, Mrundi, Emiry Nimubona, Mzimbabwe, Justive Majabvi pamoja na golikipa raia wa Ivory Coast, Vincent Angban wamesajiliwa kama nyota wa kigeni.

“Tunaweza kufikia malengo kutokana na kikosi tulichonacho” anasema mwalimu wa timu hiyo, Dylan Kerr.

Kikosi kamili ni,

Makipa: Vincent Angban, Manyika Peter Manyika, Denis Richard.

Walinzi: Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Samih Hajji Nuhu, Abdi Banda, Mohamed Hussein, Juuko Murish, Mohamed Fakhi.

Viungo: Jonas Mkude, Said Ndemla, Justice Majabvi, Emiry Nimubona, Simon Sserunkuma, Peter Mwalyanzi, Mwinyi Kazimoto, Awadh Juma.

Washambuliaji: Musa Hassan Mgosi, Daniel Lyanga, Ibrahim Ajib, Joseph Kimwanga, Boniface Maganga, Issa Abdallah, Said Issa, Emanuel Mtumbuka, Hamis Kizza, Pape N’daw.

Enyeama Aigwaya Taifa Stars
Thierry Henry Amtetea Arsene Wenger