Klabu ya Simba imeendelea kupata ushindi na kujisogeza taratibu kileleni mara baada ya kuitandika Azam FC magoli 3-1 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es salaam.
Bao la kuongoza la Simba lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 5 ya mchezo kipindi cha kwanza baada ya kupata pasi safi kutoka kwa John Boko na kumuacha kipa wa Azam FC, Razak Abarola akipigwa butwaa.
Simba waliongeza bao la pili dakika ya 38 kutoka kwa John Boko ‘Adebayor’ baada ya kupokea krosi safi iliyopigwa na Zana Coulibaly na kuifanya Simba iende mapumziko ikiwa kifua mbele kwa magoli mawili.
Aidha, Kagere aliifungia tena Simba bao la tatu dakika ya 77 na kuihakikishia kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo, huku akiibua gumzo uwanjani hapo wa namna ya ushangiliaji wake wa goli hilo.
Hata hivyo, Azam FC walizinduka kutoka usingizini baada ya kupata bao la kufutia machozi dakika ya 81, lililowekwa wavuni na Frank Domayo, ambapo mpaka mpira unamalizika Simba walikuwa tayari wamenyakua pointi 3 muhimu.
-
Mwinyi Zahera afunguka kuhusu Mbao FC
-
Simba yaikung’uta Yanga, yaanza kuunusa ubingwa
-
Simba yafufua matumaini ya robo fainali, yaichakaza Al Ahly