Klabu ya Simba imefanya mkutano wa dharura jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo, huku serikali ikibariki mabadiriko ya Katiba hiyo.
Serikari imetoa baraka hizo kupitia kwa Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akitoa neno juu ya mabadiliko hayo ambapo amesema Simba imefuata taratibu na kanuni zilizowekwa na serikali hivyo kila kitu kinfanyika kwa mujibu wa sheria.
”Mabadiliko yanayofanywa na klabu hii ni mazuri na yataleta maendeleo kwenye soka la Tanzania, hivyo hayana budi kuungwa mkono ili yakamilike kwa wakati na sisi kama serikali tutahakikisha yanafanikiwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu husika,”amesema Dkt. Mwakyembe
Aidha, Mwanasheria wa Simba, Evodius Mtawala, amefafanua namna ambavyo mfumo huo utafanya kazi kuanzia kwa mmiliki wa hisa nyingi ‘Mo Dewji’ atakayemiliki asilimia 49 ya hisa huku wanachama wakimiliki 51%.
-
Tanzania yatinga fainali kombe la dunia
-
Rais Magufuli kukabidhi kombe la Ubingwa 2017/18
-
Juma Kaseja avuruga ya rekodi Simba
Hata hivyo, kwa upande wa wanachama watamiliki hisa ndani ya kampuni ya ‘Simba Sports Club Company Limited’ kupitia kwa kampuni ya wanachama itakayoitwa ‘Simba Sports Club Holding Company Limited’ chini ya baraza la wadhamini