Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC umelitolea ufafanuzi suala la Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Maddie Kagere kutocheza wakisema hata kama ingekuwa vipi Kagere asingeingia wala Mugalu kutoka kwa vile tayari kanuni mpya za FIFA kuhusu sub za Corona zilizuia mabadiliko hayo.

Sheria hiyo inaeleza Timu moja itafanya mabadiliko ya wachezaji wake watano katika mikupuo MITATU tofauti ndani ya mchezo mmoja.

Meneja wa Simba SC Patrick Rweyemamu ameeleza kuwa Simba ilitumia mkupuo wa kwanza kwa kumtoa kiungo Mzamiru Yassin dakika ya 24 na kisha nafasi yake kuchukuliwa na winga Bernard Morrison iki kuongeza kasi ya mashambukizi baada ya kugundua Kaizer waliingia na mbinu ya kukaa nyuma.

Meneja huyo amefafanua kuwa shida ilikuja katika matumizi ya mkupuo wa PILI na watatu na tukio la kuumia kwa mpigo kwa wachezaji wao wawili kiungo Thadeo Lwanga na beki Joash Onyango ndio shida ilipokuja.

Mwanzo madaktari waliona Thadeo hataweza kuendelea na kutakiwa kutolewa haraka akaingia Erasto Nyoni, Baada ya muda tukaambiwa hata Onyango hawezi tena kuendelea na wakashauri atolewe sasa pale ndipo kila kitu kiliharibika na kama mliona kila mtu alisikitika sio tu kumpoteza Onyango lakini tuliumizwa kwa kutumia vibaya kanuni hii mpya ya mabadiliko.

Tulilazimika kumtoa Onyango na nafasi yake akaingia Kennedy Juma. Kwa hesabu mkupuo wa kwanza ulitumika kumuingiza Morrison wa Pili Nyoni na watatu Kennedy.

Ukiangalia kanuni hapo haikuwaruhusu makocha tena kumwingiza Kagere wala kumtoa Mugalu na hapo hesabu zote zikiharibika lakini kubwa ilikuwa pale walipoumia Onyango na Lwanga.

Mwinyi ateua Mkuu wa Shule ya Sheria ZNZ
Waziri Aweso: Muwe mmefika mpaka Mei 29