Baada ya kukamilisha dakika 90 za Mkondo wa Kwanza wa Mchezo wa Kuwania kufuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Power Dynamos katika Uwanja wa Levy Mwanawasa, Uongozi wa Simba SC unaipigia hesabu Coastal Union.

Simba SC juzi Jumamosi (Septemba 16) iliambulia sare ya 2-2 ugenini nchini Zambia, mabao yote ya Mnyama yakifungwa na Kiungo Clatous Chotta Chama.

Leo Jumatatu (Septemba 18) msafara wa Simba SC umerejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa mzunguko wa tatu kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Simba Ahmed Ally ameweka wazi kuwa baada ya mchezo wa kimataifa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mechi zinazofuata.

“Wachezaji wote wapo sawa kwa ajili ya mechi zetu zijazo, leo Jumatatu (Septamba 18) kikosi kimewasili Dar na hapa kitaendelea na kambi kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Coastal Union.

“Mchezo huo ratiba ya awali inaonyesha kwamba tutacheza Uwanja wa Uhuru na ipo hivyo mpaka sasa lakini kuna mazungumzo ambayo yanafanyika tutaweka wazi wapi mchezo huo utachezwa.”

Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira, Simba SC ilicheza mechi mbili ikikusanya pointi sita na mabao sita huku safu ya ushambuliaji ikitunguliwa mabao mawili.

Coastal Union ilikusanya pointi moja iliposhuhudia ubao wa Uwanja wa Manungu ukisoma Mtibwa Sugar 1-1 Coastal Union.

Mweka yatoa usaidizi kwa watoto Yatima, wenye ulemavu
Hersi Said: Hili ndilo tunalolitaka sasa