Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kumsajili mchezaji mpya raia wa Brazil, Gerson Fraga Vieira atakaye itumikia timu hiyo kwa muda wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika klabu hiyo inasema Fraga amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo ana uwezo wa kucheza nafasi ya mlinzi wa kati akiwa uwajani pamoja na kiungo mkabaji.
Klabu hiyo imesema mchezaji huyo amewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Brazil ya vijana chini ya maika 17 iliyo undwa na baadhi ya wachezaji ambao Neymar Santos,Philipe Coutinho,Casemiro, mlinda mlango Alison.
Fraga amejiunga na wekundu hao wa msimbazi akitokea katika timu ya ATK FC ya nchini India.