Leo ni siku nyingine ya kuweka historia katika medani ya soka Tanzania kupitia mchezo kati ya mahasimu na watani wa jadi, Simba na Yanga, mchezo wenye hesabu kali katika Ligi Kuu Tanzania Bara, watakapokipiga katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu zote mbili ambapo vikosi vya timu hizo vitatoka mafichoni Zanzibar vilikoenda kupiga kambi na kujifua, Yanga walikuwa Pemba wakati Simba wakiwa Unguja.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali wa kumfanya punda afe lakini mzigo uende kwa sababu timu zote zinahitaji pointi tatu muhimu kuipa nguvu za kuelekea kileleni kwa ligi hiyo. Yanga ambayo iko kileleni mwa ligi hiyo kwa pointi 9 ikiongoza kwa idadi ya magoli dhidi ya Simba na Azam zenye pointi 9 pia, itatifua mbio zaidi endapo itashinda. Lakini Endapo Mnyama atawavuruga wana Jangwani hao atapaa na kuongoza ligi.

Matokeo ya sare yoyote kati ya timu hizo yatatoa nafasi zaidi kwa Azam Fc hasa pale itakaposhinda katika mchezo kati ya timu hiyo na Mbeya City, utakaofanyika katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

 

Nay Wa Mitego Amvaa Rasmi January Makamba Kuitetea Ukawa
Magufuli Apotezea Majibu Ya Tafiti, Awaonesha Wananchi Njia Mbadala