Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Klabu ya TP Mazembe, Deo Kanda kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja..

Mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa Congo DR, mwenye umri wa miaka 29 amejiunga na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo inasemekana kuwa ndiye mrithi wa Emanuel Okwi.

Kanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Msimbazi akitokea TP Mazembe, ambapo alikuwa mmoja kati ya wachezaji walioiwezesha timu hiyo kushinda ubingwa wa Afrika.

Aidha, Kanda alifunga pia goli kwenye mchezo wa fainali ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Esperance mwaka 2013.

Mshambuliaji huyo pia ameshiriki Kombe la Dunia la vilabu mwaka 2009, 2010, 2013. Mwaka 2010 walifika fainali na kufungwa 3-0 na Inter Milan.

Aliyezamia kwenye ndege aripotiwa kufariki Dunia baada ya kudondoka
Membe akerwa na suala la utekaji, 'Lisipokemewa litafika mpaka kwenye uchaguzi'

Comments

comments