Mabingwa wa soka Tanzania Bara Wekundu wa Msimbazi Simba wametuma salamu za pomgezi kwa Rais wa Jamuhuri wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Simba SC wamewasilisha salamu hizo za pongezi saa chache baada ya Rais Samia kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam, na kuwa Rais wa awamu ya sita ta Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, akitanguliwa na Hayati John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia Machi 17.

Katika salamu za pongezi kutoka kwenye klabu hiyo inayoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, imemtakia kila la kheir Rais Samia kwenye majukumu yake ambayo yanaanza rasmi leo Ijumaa (Machi 19).

Klabu ya Young Africans nayo imetuma salam za pongezi kwa Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuweka ujumbe maridhawa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Magufuli kuzikwa Machi 25
Samia Suluhu Rais wa sita wa Tanzania