Wakala wa Barabara mjini na Vijijini (Tarura) Mkoa wa Simiyu, umeomba uongozi wa mkoa huo kusaidia kupata fedha zake ambazo wanazidai halmashuari ya wilaya ya Meatu pamoja na Bariadi vijijini.

Ombi hilo limetolewa jana Desemba 15, na Mratibu wa wakala huo mkoa Mhandisi Dk. Philimoni Msomba, wakati wa kikao cha bodi ya barabara mkoa, ambapo amesema wanazidai halmashuari hizo zaidi ya Sh milioni 134.

Msomba amesema kuwa katika halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Tarura inadai zaidi ya Sh milioni 97.5 huku Bariadi Vijijini wakidai zaidi ya Sh milioni 37.1, fedha ambazo amesema wamezidai toka mwaka 2017.

Dkt. Mwinyi avunja bodi ya Wakurugenzi

“Halmashauri hizi zilitumia fedha hizi kutoka mfuko wa barabara, baada ya tarura kuanzishwa tulikuta tayari wamezitumia, tukaendelea kuwadai lakini mpaka leo bado hawajazirejesha, tunaomba viongozi wa mkoa, mtusaidia tupate fedha hizi ili tuwalipe wanaotudai,” amesema Msomba.

Katika kikao hicho Mratibu huyo amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/21, Tarura imepanga kutumia Sh bilioni 5.1 kwa ajili ya ukarabati wa madaraja pamoja na barabara kilometa 822.

Afungwa maisha kwa kumlawiti mwanae

EU yatoa msaada kwa Tanzania bilioni 84
Marekani : mshirika wa Trump ampongeza Biden