Beki wa AC Milan, Simon Kjaer amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kufuatia kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Inter Milan kwenye mechi ya Serie A, uliopigwa mwishoni mwa juma lililopita (Jumamosi –Septemba 16).

Kichapo hicho kizito kimewashangaza mashabiki lakini beki huyo amewaomba radhi na kuwataka kuiamini timu yao licha ya kichapo hicho.

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika beki huyo alisema mechi za dabi zina ushindani mkali lakini Inter ilikuwa bora zaidi.

“Matokeo kama haya kwenye dabi yanachanganya sana. Nawaomba radhi mashabiki, Inter ilikuwa hatari zaidi. Tulipambana mpaka tulipofungwa mabao matatu. Ni safari ndefu na tunatakiwa kupambana.

“Inter ilitengeneza nafasi nyingi, biyo ni staili yao ya uchezaji. Walicheza vizuri sana kuanzia sehemu ya kiungo,” alisema beki huyo

Inter iliweka rekodi tamu ya kuifunga Milan mabao matano kwenye Uwanja wa San Siro kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1967.

Vijana wa Simone Inzaghi walionekana kuwa tishio dhidi ya Milan ambayo ilianza kufunga bao la kwanza dakika ya tano ya mchezo huo, bao hilo liliwekwa kimiani na Henrikh Mkhitaryan kabla ya kupachika bao jingine.

Mabao mengine ya Inter yalivwekwa kimiani na Davide Frattesi, Hakan Calhanoglou na nyota mpya aliyesajiliwa Marcus Thuram, bao pekee la AC Milan liliwekwa kimiani na beki wa kimataifa wa Ureno, Rafael Leao hata hivyo, halikutosha kuizuia Inter kutamba na kichapo hicho.

Bunge la Tanzania, Morocco kuunda ushirikiano
Kumzika Lokassa ya Mbongou Dola elfu 10