Hatimaye Mshambuliaji hatari wa Kitanzania, Simon Msuva ametambulishwa kuwa mchezaji mpya wa JS Kabylie ambayo mashabiki wake wanatamba huko Algeria kupitia mitandao ya kijami.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Mshambuliaji huyo wa zamani wa Wydad Casablanca ya alifanyiwa vipimo vya afya ambavyo alifuzu, na sasa ni rasmi amekamilisha usajili wake.

Sallah Gentlmen ambaye ni mmoja wa mashabiki hao anaamini kwa ubora wa mshambuliaji huyo ni wazi kuwa msimu ujao watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Algeria.

“Nimetazama video zake nimeona kuwa ni mshambuliaji mwenye uzoefu ambaye anaweza kuongeza kitu kwenye timu, Tunasubiri kuona akitupa raha.” Mohamned Khalef alisema

Vyombo mbalimbali vya Algeria vimeripoti juu ya Msuva kuwapo huko, huku akitangazwa kujiunga na JS Kabyie anbayo imewahi kutwaa Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili.

Man Utd yampigia hesabu Marcos Alonso
Samatta kucheza Makundi Europa Conference