Winga wa timu ya Taifa ya Tanzania Saimon Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Agosti katika klabu yake ya Difaa Al Jadid inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Msuva ambaye alijiunga na Difaa Al Jadid miezi miwili tu iliyopita akitokea Yanga ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti kutokakana na mchango wake mkubwa kwenye timu hiyo.

Tayari Msuva ameonekana kuwa tegemeo katika upachikaji wa mabao katika kikosi cha Difaa Al Jadid iliyoshika nafasi ya pili msimu uliopita na mshambuliaji huyo ataisadia klabu yake katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Kiwango cha Simon Msuva kiuchezaji kimeongezeka kwani winga huyu ameonyesha kuwa kwenda nje kuna faida yake.

Tangu ameenda nje na kurejea katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana, ameonyesha ni mchezaji ambaye ameongezeka vitu katika miguu yake kwani aliweza kuifungia Stars mabao mawili.

 

 

Video: Lissu hali bado tete Nairobi, Vita ya Spika Ndugai, Zitto yapamba moto
Mwanasiasa maarufu atekwa nchini Burundi