Mchezaji wa timu ya Yanga, Simon Msuva hivi karibuni amepata mualiko kwenda kuichezea timu ya klabu ya Morocco, hayo yamezungumzwa na Kaimu Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga , Anderson Chicharito.

Msuvaa ameonesha kutokuwa tayari kuingia makubaliano na timu hiyo klabu ya Morocco kutokana na sababu za kimasilai, ambapo yeye alitarajia kulipwa kikwango kikubwa zaidi kuliko kiwango ambacho klabu hiyo kimetaja kumlipa Simon Msuva.

Kwa taarifa iliyotolewa, klabu hiyo imepanga kumlipa Msuva mshahara wa dola za Marekani 4,000 ambazo ni sawa na takribani milioni 9 za kitanzania.

Ukiachia mbali wito huo wa klabu ya Morocco, Msuva pia amekua akiitwa na kuwindwa na timu za nchi nyingine kama vile Misri na Afrika kusini baada ya kuvutiwa na kiwango cha uchezaji wa nyota huyo.

Kwa sasa Msuva yupo Afrika Kusini kikosi cha Taifa Stars ambacho jana kilicheza mchezo wa kutafuta ushindi wa tatu dhidi ya Lesotho, baada ya kushindwa kuingia fainali kutokana na kufungwa na klabu ya Difaa El Jida.

 

Hivyo wanamsubiri arejee ili waweze kukaa chini kwa ajili ya pande zote kufikia makubaliano.

Ripoti ya PAC yaanika vigogo, wanasiasa na viongozi wa dini upigaji hela za Escrow
Video: Coyo afunika na video mpya 'Itakucost', iangalie hapa