Baada ya kuthibitika beki Juma Abdul atakosekana kwenye kikosi cha Young Africans kitakachopambana na Mo Bejaia katika mchezo hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF, utakaochezwa mwishoni mwa juma hili nchini Algeria, mshambuliaji wa klabu hiyo Simon Msuva, ameonyesha kuwa na matumaini na beki wao mpya, Hassan Kessy ataziba pengo beki wa kulia  kikamilifu.

“Asikuambie mtu Kessy ni bonge la beki, anajua kupandisha mashambulizi vizuri na pia ni mtaalamu kwenye upigaji wa krosi zinazozaa mabao.”

“Hata kama kikosi chetu kitamkosa Juma Abdul, bila shaka kwa uwezo alionao Kessy tutafanya vizuri na kufikia malengo yetu. Nimecheza nae kwenye timu ya taifa anajua jinsi ya kupima na kupiga krosi ambazo naamini zitatupa mabao dhidi ya Mo Bejaia,” alisema Msuva.

Mara ya mwisho Kessy kucheza kwenye kikosi kimoja na Msuva mwezi  Desemba, mwaka jana wakati wakiwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), iliyokuwa ikishiriki michuano ya Chalenji na wawili hao walionekana kuwa na uelewano mkubwa.

Mashabiki Wamnanga Anthony Martial Katika Mtandao Wa Twitter
Video: Uwanja aliopigia push up Rais Magufuli umefikishwa Bungeni na Mbunge Bashungwa