Kikosi cha Singida Big Stars kipo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya JKU ya Zanzibar unatakaochezwa kesho Jumapili (Agosti 27) kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Afisa Habari wa Klabu hiyo Hussein Massanza, amesema wamewasili Dar baada ya kucheza mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Prisons na kutoka suluhu katika Uwanja wa Liti, Singida, akibainye Uwania

Masanza amesema kikosi chao kipo tayari na wanafahamu mchezo huo utakuwa ngumu kwa sababu mpira siku zote una matokeo katili na ya ajabu, lakini kwa hali ya kawaida tu ni kwamba wana matumaini makubwa ya kusonga mbele na kwenda kukutana na Future ya Misri.

Hata hivyo Massanza amewaonya JKU wasijidangaye kudhani wanaweza kushinda mabao 3-0 kiurahisi kwani wamejipanga kwa kila njia kuhakikisha wanalinda Ushindi wao wa mabao 4-1 walioupata awali.

Mwishoni mwa juma lililopita Singida Big Stars ilishinda idadi hiyo ya mabao kwenye Uwanja huo huo ambao washindi walikuwa nyumbani.

JKU nayo itautumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani na mshindi wa jumla atakwenda kucheza raundi ya kwanza dhidi ya Future ya Misri, Septemba 15 nyumbani, kabla ya kwenda kukabiliana nayo Ugenini mechi ya mkondo wa pili, Septemba 29.

Mauricio Pochettino kusajili wawili Chelsea
lvan Toney aziingiza vitaji Arsenal, Spurs