Uongozi wa klabu ya Singida Big Stars umefikia makubaliano ya kuiuza timu hiyo kwa wamiliki wa Fountain Gate.

Mtendaji Mkuu wa Singida Big Stars John Kadutu amesema hayo mkoani Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Amesema wameridhia kuiuza timu hiyo kwa Fountain Gate, lakini kwa sharti la timu hiyo kubakia mkoani Singida.

TAARIFA ya Singida Big Stars imesema: “Tunapenda kuwataarifu wadau na mashabiki wetu kwamba uongozi wa Singida Big Stars FC umefanya makubaliano ya kibiashara ya kuuza hisa zake kwa uongozi wa Fountain Gate Academy.”

“Makubaliano hayo yameambatana na baadhi ya mabadiliko katika uendeshaji wa klabu kwa upande wa Bodi na Menejimenti.”

“Pia tumebadilisha jina kutoka Singida Big Stars FC kuwa Singida Fountain Gate FC (The Big Stars).”

Kwa upande wake Mmiliki mpya wa Timu hiyo Japhet Makau amesema, fursa hiyo imekuja katika wakati muafaka ndio maana wamemua kuichangamkia.

Kwa sasa jina la Singida Big Stars limebadilishwa na kuitwa Singida Fountain Gate Football Club.

Vinicius akabidhiwa namba ya kazi Real Madrid
Dani Cadena apewa mkono wa kwaheri Azam FC