Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ limeifungia Klabu ya Singida Fountain Gate FC kusajili hadi itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo ya mjini Singida  Pascal Serge Wawa.

FIFA imefikia uamuzi huo baada ya Wawa kushinda kesi ya madai aliyoifungua katika shirikisho hilo dhidi ya waajiri wake wa zamani.

Beki huyo kutoka nchini lvory Coast alifungua kesi ‘FIFA’ akidai malipo ya ada ya usajili (sign on fee) na malimbikizo ya mishahara kwa mieizi kadhaa.

Hata hivyo Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa Beki huyo ambaye aliwahi kuzitumikia Azam FC na Simba SC zote za Tanzania, ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Wakati FIFA ikitangaza kuifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.

Wakati huo huo TFF imezikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

Simba SC yatahadharishwa Morocco
Wajadiliana kuimarisha nafasi ya Wanawake katika Uongozi