Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Singida Fountain Gate FC imeanza mikakati kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ pamoja na Mochuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la SOka Barani Afrika ‘CAF’.

Bodi hiyo jana Jumatano (Juni 28) ilikutana kupitia ripoti ya kocha Hans van der Pluijm ambapo mbali na mambo mengine pia imejadili eneo la kuweka kambi timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Msemaji wa timu hiyo Hussein Masanza amesema moja kati ya mambo ambayo yalijadaliwa ni pamoja na usajili wa maboresho kwenye timu hiyo.

“Leo Alhamis (Juni 29) kikao kitaendelea na baada ya kumalizika tutajua timu itaweka kambi wapi na kuweka wazi mikakati yetu kuelekea msimu mpya, lengo la bodi ni kuona timu inafanya vizuri zaidi msimu ujao,” amesema Masanza.

Amesema wamepanga kufanyia maboresho makubwa katika safu ya Ulinzi, Ushambuliaji, Kiungo wa pembeni na kati kusajili wachezaji wenye viwango vya juu ili kuwapa burudani mashabiki wao.

“Tunawachezaji wengi wazuri kwenye safu hizo lakini tunataka kuongeza nguvu zaidi ili tufanye vyema kwenye michuano ya Kimataifa,” amesema Masanza.

“Pia tuna malengo ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, usajili wetu pia utalenga maeneo hayo, mashabiki na wapenzi wa timu yetu wasubiri kuona mabadiliko makubwa,” amesema Masanza.

Amesema wamepania kuhakikisha msimu ujao wanafanya vizuri na wana kikosi ubingwa basi washike nafasi za juu zitakazowapa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa kama ilivyo msimu wa 2022/23.

Mabaki ya miili ajali ya Nyambizi Titan yapatikana
Rada za Man Utd zamsoma Frenkie de Jong