Bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Danny Usingimana katika dakika ya 82, limetosha kuipa ushindi wa kwanza Singida Utd katika uwanja wao wa nyumbani wa Namfua, uliopo mjini Singida dhidi ya Lipuli FC leo jioni.

Mchezo huo wa mzunguuko wa kumi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara ulionekana kuwa ni wavuta ni kuvute wakati wote, huku Singida Utd wakionyesha kuwa na hitaji kubwa la kuibuka na ushindi, baada ya kuanza kwa matokeo ya sare kwenye uwanja wa Namfua dhidi ya Young Africans majuma mawili yaliyopita.

Katika kipindi cha pili Singida Utd waliokua wanacheza mbele ya mashabii wao, walionekana kuwa wakali zaidi kwa kulishambulia lango la Lipuli FC, lakini asilimia kubwa ya mashambulizi yao hayakufanikiwa kutinga katika nyavu za wageni.

Hata hivyo Lupuli FC nao walijaribu kulishambulia lango la Singida Utd kwa kushtukiza mara chache, lakini mashambulizi yao yalikabiliwa vilivyo na safu ya ulinzi ya Singida Utd.

Kufuatia ushindi huo, Singida Utd wanafiisha point 17 sawa na Mtibwa Sugar ambao watashuka dimbani mwishoni mwa juma hili kucheza na ndugu zao kutoka mkoani Kagera (Kagera Sugar), katika uwanja wa Manungu Complex huko wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Michezo mingine ya mzunguuko wa kumi ya ligi kuu ya soka Tanzania bara itachezwa kesho ambapo, maafande wa jeshi la Magereza Tanzania Prisons watakua nyumbani mkoani Mbeya wakipepetana na wekundu wa Msimbazi Simba kwenye uwanja wa kubukumbu ya Sokoine.

Mkoani Pwani eneo la Mlandizi, maafande wa Ruvu Shooting watawakabili Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara katika uwanja wa Mabatini, ili hali mkoani Ruvuma katika mji wa Songea Majimaji FC watakua wenyeji wa Mbao FC kutoka mkoani Mwanza.

Mkoani Shinyanga Stand Utd watakua nyubani katika uwanja wa kambarage kukabana koo na ndugu zao kutoka wilaya ya Kishapu Mwadui FC.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 18, 2017
Video: Nairobi yageuka uwanja wa vita mapokezi ya Odinga