Taarifa za hivi punde ni kwamba Singida imeimarisha safu ya Ushambuliaji kwa kuongeza washambuliaji Kambale Salita (Papy Kambale) na Danny Lyanga huku wachezaji wawili wakitalajiwa kutangazwa hivi punde.

Katika hatua za kuendeleza mpira nchini, klabu ya Singida United imewasaka na kuwapata vijana wanne walioshiriki Michuano mikubwa barabi Africa kwa vijana umri chini ya miaka 17 AFRICON 2017 waliokuwa na kikosi cha Serengeti Boys.
Hatua hiyo ni moja ya mipango iliyowekwa na uongozi wa kusaidia vijana hasa wale ambao walishaonekana na hata kulipigania Taifa na baada ya michuano hiyo kumalizika wengi wao walitawanyika na kukosa timu za kusimama nao.

Hivyo katika kulinda vipaji hivyo, Singida United imeamua kuchukua wachezaji wa nne kwa usajili wa miaka mitatu kila mmoja huku wakilipwa Signing fee,mshahara na allowance stahiki zao ili kuwajenga katika mfumo wa soka la ushindani.

Vijana hao,mmoja ni kepteni wa Serengeti Boys Ndg.Issa Makamba kiungo wa kati,Mwingine ni Assad Juma mshambuliaji nimzaliwa wa Zanzibar, pia Ally Ng’azi beki na Mohamed Abdallah mshambuliaji.

Mawakili watakiwa kujiajiri
Uganda yatepeta kwa Zanzibar Heroes