Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) Tundu Lissu, amesema kuwa kuwa makundi ya watu yanayojitokeza katika kampeni zake hana uhakika kama wote wamejiandikisha kwa sababu wagombea huwa hawaulizi wapiga kura iwapo wamejiandikisha.

Lissu ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 26, 2020, wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Mwanza, na kuongeza  kuwa CHADEMA ya 2020 si kama ile ambayo ilisimamisha wagombea katika uchaguzi kwa miaka iliyopita akiwemo Dkt Slaa na Edward Lowassa kwa kuwa sasa hivi chama hicho kina matawi kila mahali.

“Haya makundi ya watu yanayokuja katika mikutano yetu hatujui kama wanaokuja kwenye mikutano wamejiandikisha kwa sababu hatuwaulizi, katika siasa mtaji ni watu, ukitaka kujua mwanasiasa anaungwa mkono kiasi gani ni watu, ukiona mtu anafanya mkutano wanahudhuria watano ujue huyo hana lolote kwenye ulingo wa siasa,” amesema Lissu.

 “Kuna tofauti kubwa kati ya Mrema mwaka 1995, Slaa wa 2010 na Lowassa wa 2015, tofauti kati ya Tundu wa 2020 ni kubwa sana na tofauti yake sasa tuna ‘organisation’ na ndiyo maana tuko kila mahali kwahiyo tuna uwezo wa kuweka mawakala nchi nzima, uwezo huo hatukuwa nayo miaka ya nyuma, na tuna matawi kila mahali,” ameongeza Lissu.

Togo: Waziri mkuu na serikali yake wajiuzulu
“Nimesikitishwa sana”- Kikeke