Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus, wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa pembeni  kutoka nchini Brazil na klabu ya Atletico Madrid, Guilherme Siqueira.

Beki huyo wa kushoto, kwa kipindi kirefu alikua anawaniwa na Juventus, na tayari imeelezwa kwamba mipango hiyo inakaribia kukamilishwa baada ya viongozi wa klabu hizo mbili kufikia makubaliano ya kufanya biashara.

Siqueira mwenye umri wa miaka 29, atajiunga na klabu ya Juventus kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu wa 2015-16, na endapo atawaridhisha wahusika wa benchi la ufundi klabuni hapo, huenda akasajiliwa moja kwa moja.

Tovuti ya Tuttosport imeripoti kwamba, ada ya usajili wa mkopo kwa kwa beki huyo ni Euro million 1.8, na kama atauzwa moja kwa moja mwishoni mwa msimu ataigharimu Juventus, Euro million 6.

Tovuti hiyo imeongeza kwamba, kama mambo hayo yatakwenda vyema, Siqueira atasajiliwa na Juventus kwa mkataba wa miaka miwiwli na kwa kila mwaka atakua akilipwa Euro million 2.

Tetesi Za Usajili Barani Ulaya
Mwigulu Nchemba Awataka Watanzania Kumuogopa Lowassa