Serikali nchini Sri Lanka imepiga marufuku vazi linalofunika uso “nikabu” kuvaliwa na wanawake nchini humo kufuatia shambulio la mabomu siku ya pasaka lililo pelekea vifo vya watu 250 na kujeruhi mamina ya watu waliokuwa ndani ya makanisa na hoteli.

Rais wa nchi hiyo Maithripala Sisirsena amesea kuwa ametumia sheria ya dhalula kupitisha zuio hilo litakaloanza kufanyakazi leo jumatatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake imeeleza kuwa vazi lolote ambalo linaficha sura ya mtu halita ruhusiwa nchini humo ili kuimarisha usalama wa nchi.

Nchi ya Sri Lanka imekuwa katika hali ya tahadhari ya juu siku nane baada ya shambulio la mabomu lililotekelezwa na kikundi cha waislam wenye msimamo mkali ambapo tayari washukiwa wamekamatwa na polisi wanaendelea na ulinzi mitaani.

Nchi hii ina wakazi zaidi ya milioni 21 na asilimia 10 ya wakazi hao ni waumini wa dini ya kiislam, na zuio la kuvaa nikabu lilipendekezwa na mbunge wiki iliyopita.

Siku za mapumziko ya wiki wanajeshi wa Sri  Lanka walimarisha ulinzi mkali katika makanisa na misikiti huku ibada za jumapili zikiwa zimezuiliwa kufanyika nchi nzima na kanisa pekee lililo kusanya waumini ni la Mtakatifu Anthony ambalo pia lilipigwa bomu siku ya pasaka.

Idadi ya watu waliokamatwa kwa kuhusishwa na shambulio hilo imefikia 150, na mamlaka nchini humo bado inaendelea kuwatafuta wafuasi 140 wa kikundi cha Jihadi kilicho kili kuhusika na shambulio.

Kambi za Kitaaluma mkoani Simiyu ni za kudumu- RC Mtaka
Mwanamitindo apoteza maisha stajini

Comments

comments