Uongozi wa Soka mkoa wa Singida umethibitisha kukamilika kwa maandalizi ya mchezo wa pili wa Nusu Fainali, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kati ya Singida Big Stars dhidi ya Mabingwa watetezi Young Africanas.

Timu hizo zitapambana Mei 07 katika Uwanja wa CCM Liti mjini Singida, ukitanguliwa na mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya ASFC utakaopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC Mei 06.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Singida ‘SIREFA’ Hamis Kitila amesema maandalizi ya mchezo wa Singida Big Stars dhidi ya Young Africans yanakwenda viziri na hadi sasa yamefikia zaidi ya asilimia 90.

Kitila amesema hali ya Uwanja upo shwari na taratibu nyingine za nje ya Uwanja zipo katika mpango mzuri, hivyo amewataka Mashabiki wa soka mkoani Singida na mikoa ya karibu kufika kwa wingi ili kushuhudia mchezo huo utakaoanza saa tisa alasiri.

“Uwanja upo vizuri utaratibu wa upatikanaji wa tiketi tutauweka vizuri, kikubwa ni mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani,” amesema Kitila.

Young Africans itacheza michezo miwili ndani ya juma moja mkoani humo ikianza na Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ itakayochezwa Mei 04 na Mei 07 itacheza mchezo wa Ligi Kuu.

Singida Big Stars itacheza Nusu Fainali hiyo baada ya kuifunga Mbeya City mabao 4-1 mchezo wa Robo Fainali uliofanyika Uwanja wa Liti huku Young Africans ikiifunga Geita Gold bao l-0 Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Upande wa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu uliofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, Singida Big Stars ilikubali kichapo cha mabao 4-1.

Singida Big Stars inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 51, imeshinda michezo 15 na kufungwa mitano huku Young Africans ikiongoza kwa kuwa na alama 68.

Uongozi Simba SC waapa kuandika rekodi Afrika
Polisi yawadaka 132 silaha haramu, mimba za Wanafunzi