Msemo wa wahenga ‘Mtoto wa nyoka ni nyoka’, umeendelea kutumiwa sana katika jamii zote ndani na hata nje ya mipaka ya Tanzania, ingawa kuna watoto wanyoka wengine ambao hugeuka kuwa kenge nafasi ya Mzazi katika kuhakikisha mwanaye anafuata nyayozake ni muhimu sana.
Joyce Msuya, mtoto wa waziri mkuu msaafu Cleopa Msuya ambaye kwasasa ndiye naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la mazingira, UNEP na mwanamke wa kitanzania aliyeteuliwa Mei 21, 2018 na Katibu mkuu wa UN, Antonio Gutteres, ameeleza siri iliyomfanya apate nafasi hiyo ya uongozi wa juu.
“Sikuota kufika hapa, lakini nilifanya kazi kwa bidii sehemu nyingi kujiandaa na majukumu ya juu”, Joyce ameliambia mwananchi baada ya kuhudhuria mkutano wa mazingira wa UN uliofanyika jijini Nairobi Machi 11 hadi 15, kujadili masuala mazingira na athari zake.
Joyce ameeleza kuwa alikuwa kati ya watu 100 walioona tangazo la kumsaka naibu mkuurugenzi mtendaji wa Unep, wakaomba na baadae kuchujwa hadi kufika tisa kutoka matifa tofauti, ambapo yeye kwa upande wake alisailiwa kwa njia ya video “video conference”. na kufanikiwa kupata nafasi hiyo.
Licha ya kutokea kwenye familia ya waziri mkuu msaafu, Cleopa Msuya, ambaye angemuwezesha kupata nafasi za juu kirahisi, Joyce amesema hakujari anaamini katika kufanya kazi kwa bidii ili kufanikiwa.
“Daima naamini kufanya kazi ngumu na tofauti ili nijifunze na kukua kitaaluma, ni kwasababu hii nilishindana na kufanikiwa kuchaguliwa kwenye kazi za China, Korea Kusini na hapa Unep” ameelza Joyce na kuongeza “tuzoee kufanya kazi na vitu vigumu ambayo vinaweza kututofautisha na wengine, pale tutakapo shindwa, tujiulize kwanini hatukufanikiwa ili tujifunze na kusonga mbele”.
Ni mama wa watoto wawili, Melanie na Ethan, na amesisitiza kuwa kupata nafasi hiyo ya sasa kunatokana na juhudi na uthubutu wa kujaribu mambo magumu ili kukua kitaaluma, na kupata upeo mpana wa maisha, binadamu na mataifa tofauti.
Lakini pamoja na juhudi hizo Joyce anasema kuwa familiya yake kuanzia mume wake, watoto pamoja na wazazi wake wanamchango wao, hasa katika kumshika mkono katika kila hatua na malezi bora aliyoyapata.
“Wazazi walinifundisha kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu watu wote na kutosahau nilipotoka, hii ni kuanzia nyumbani kwetu Usangi, kama usengekuwa mwongozo wenye upendo wa marehemu mama yangu, Rhoda na baba Cleopa Msuya, huenda nisingefika nilipo” joyce amesema
Aidha ametoa wito kwa wanawake wa Tanzania kuwa fursa ya wanawake wengine kufikia ngazi aliyopo ipo wazi au zaidi ya hapo alipo ila nilazima wafanyekazi kwa bidii na kupata elimu ya juu kadri inavyowezekana, kwani changamoto zipo kila mahali haitakiwi kukata tamaa.
-
Bosi wa Takukuru afikishwa kortini
-
Jengeni tabia ya kupima afya mara kwa mara- Samia Suluhu Hassan
-
Ndege nyingine ya Boeing yatua kwa dharura
Joyce Msuya, Alizaliwa januari 2, 1968 jijini Dar es salaam katika hospitali ya Ocean Road, elimu ya msingi alipata katika shule ya Frodhani na baadaye kwenda shule ya sekondari Jangwani, ambako alisoma miezi sita kabla ya kuhamishiwa weruweru ambako alisoma hadi kidato cha sita.
Alijiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Muhumbili (Muhas) alikohitimu masuala ya ufamasia.
Pia ni mhitimu wa sayansi ya viumbe wadogo kutoka chuo kikuu cha Strathcyde nchini Scotland, ana shahada ya Umahiri (Microboilogy and immunology) kutoka chuo kikuu cha Ottwa nchini Canada na ana shahada ya uzamivu (PHD) kutoka chuo kikuu cha British Columbia nchini Canada.
Elimu hiyo pia imemsaidia kushika nafasi za juu katika mashirika makubwa Duniani kwani kabla ya uteuzi huu wa sasa alikuwa mwakilishi maalumu wa Benki ya Dunia na mkuu wa ofisi ya JamhurI ya Korea, Mratibu wa kanda wa Taasisi ya Benki ya Dunia iliyokuwa na ofisi zake nchini China.