Siri ya Beki wa Kushoto kutoka DR Congo Joyce Lomalisa Mutambala kuomba kuvunja mkataba na Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans imefahamika.

Beki huyo mwenye uwezo mkubwa wakupiga krosi, mwishoni mwa juma lililopita alitajwa kuuandikia barua Uongozi wa Young Africans ya kuomba mkataba wake wa mwaka ambao ameubakisha klabuni hapo uvunjwe.

Hiyo ikiwa siku chache zimebakia kabla ya usajili mkubwa wa msimu ujao kufunguliwa, ili timu shiriki za Ligi Kuu Bara zianze kufanya usajili wake.

Mmoja wa Mabosi wa Benchi la Ufundi la timu hiyo, amesema sababu kubwa ya beki huyo kuomba kuvunja mkataba ni kutofurahia kuwekwa benchi na kiraka Kibwana Shomari anayemudu kucheza nafasi zote za beki wa pembeni.

Bosi huyo amesema kuwa Lomalisa anataka kuondoka hapo ili aende kwingine akapate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, lakini sio kuendelea kubakia hapo awekwe benchi na Kibwana.

Ameongeza kuwa uongozi umekubali kumuachia beki huyo aondoke, lakini kwa sharti la kuiita mezani klabu anayotaka kwenda kwa ajili ya kufanya mazungumzo rasmi.

“Uongozi tayari umemwambia kuwa upo tayari kumuachia aondoke hapo, lakini hiyo timu inayomtaka ije kwa uongozi wa Young Africans kwa ajili ya mazungumzo.

“Kwani sababu yake inayomfanya avunje mkataba ya kitoto, kikubwa yeye kama anataka kucheza katika kikosi cha kwanza aongeze bidii ya kupambana uwanjani kila atakapopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

“Kibwana amekuwa akianza katika kikosi cha kwanza katika msimu huu uliomalizika kutokana na kiwango bora ambacho anachoendelea kukionyesha, amekuwa akitimiza majukumu yake.

Wahifadhi kuwatumia Wanasiasa kuitangaza sekta ya utalii
Haji Manara kuiponza SAMAKIBA?