Rafiki wa kike wa mlinda mlango wa Man Utd, David De Gea amefichua siri ya mustakabali wa usajili wa rafiki yake, ambaye amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kurejea nyumbani mjini Madrid kujiunga na klabu ya Real Madrid.

Edurne Garcia, rafiki wa mlinda mlango huyo, alionekana katika kituo cha televisheni huko nchini Hispania usiku wa kuamkia hii leo akifanyiwa mahojiano, na alipoulizwa ukweli wa mambo kuhusu uhamisho wa De Gea alifunguka bila uoga.

Edurne, alisema ni kweli De Gea ana matarajio makubwa ya kurejea nyumbani Madrid, na anaamini hakuna litakalo shindikana  kufuatia yeye mwenyewe kuhitaji kucheza katika klabu kubwa kama Real Madrid.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 29, alisema mara kadhaa amekua akishaurina na rafiki yake na muafaka ambao umekua ukipatana baina yao ni kubadilisha amzingira ya nchini England.

Viashirio vya kuondoka kwa De Gea katika klabu ya Man Utd vimeshaanza kuonekana baada ya kusajiliwa kwa mlinda mlango kutoka nchini Argentina, Serigo Romero na tetesi zinasema huenda akaanzishwa katika kikosi cha kwanza kitakacho pambana na Tottenham mwishoni mwa juma hili.

Taarifa nyingine zinadai kwamba endapo dili la De Gea kuelekea Real Madrid litakamilishwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba 02, Man Utd watafanya kila mbinu za kumng’oa mlinda mlango kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Spurs, Hugo Lloris.

Oliseh Amfungia Safari Mshambuliaji Wa Liverpool
Lipumba Ang'atuka CUF