Kiungo Cesc Fàbregas ametajwa katika gazeti la The Guardian kuwa ametumika kwa kiasi kikubwa kumshawishi mshambuliaji wa FC Barcelona Pedro Rodríguez kukataa mpango wa kusajiliwa na Man Utd na badala yake akubalia kujiunga nae huko Stamford Bridge.

Fàbregas ambaye ni rafiki wa karibu wa Pedro anadaiwa kufanya hivyo mara kadhaa, huku nyuma ya pazia ikidhaniwa huenda Mourinho alikua akihusika kutokana na hitaji la mshambuliaji alilokuanalo tangu mwanzoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, alifanikisha mpango huo kwa njia ya mazungumzo ya simu na inadaiwa alikua akimueleza Pedro, sifa kadhaa za klabu ya Chelsea na kuiponda Man Utd ambayo ilikua ikitajwa kuwa katika mpango mzuri wa kumsajili mshambuliaji huyo.

Hata hivyo gazeti hilo halijaainisha kwa kina uwepo wa meneja wa Jose Mourinho, kwenye ushawishi huo zaidi ya kudhani alitumika kumshawishi Fabregas kufanya hivyo.

Mourinho, inadaiwa alikua mstari wa mbele kukamilisha mpango wa kuingilia mazungumzo yaliyokua yakiendelea baina ya viongozi wa FC Barcelona na Man Utd, na hatimae alifanikiwa.

Jana mishale ya mchana kwa saa za Afrika mashariki, baadhi ya vyombo vya habari barani Ulaya viliripoti taarifa za Pedro kuikacha Man Utd na kukubali kuelekea Chelsea kwa ada ya paund million 21.2.

Kwa sasa inadaiwa Pedro yupo njiani kuelekea jijini London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na kama mambo yatamuendea vyema atakamilisha usajili wake ndani ya saa 24 zijazo.

Mapenzi Ya Jokate Yawaunganisha Ali Kiba Na Ice Prince
Otamendi Akamilisha Ndoto Za Kucheza England