Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam, IGP Simon Sirro ametoa onyo kali kwa watu wote wanaotumika kuliteteresha jeshi la polisi na kufanya serikali ya Tanzania ionekane imeshindwa kufanya kazi yake ikiwa pomja na kuwalinda watanzania.
Sirro amesema kuwa wale wote wanaopingana na kile kinachofanywa na serikali ikiwa ni pamoja na kulifundisha jeshi la polisi kazi wanajenga uadui mkubwa na majeshi na kutoa onyo kuwa watu wa namna hiyo hawatakuwa salama sababu wanatumika hivyo jeshi la polisi lipo tayari kukabiliana nao kwani watu wa aina hiyo hawana thamani kuliko Tanzania.
Kuna watu ambao ‘either’ kwa kutumwa au kwa faida yake binafsi wanataka nchi yetu isikalike ionekana serikali yetu imeshindwa lakini niwaambie hao ndugu zao wanaowatuma hawatapata nafasi sisi tupo imara wananchi wapo imara na ndio maana unaona hata mauaji yanapofanyika kibiti watu wetu wanakufa wengine wanafurahia unaweza kujiuliza hawa watu tupo nao.
Hebu waandishi wa habari fikirieni siku 9 askari wanazunguka wanaingia apartmet moja wanaingia nyingine wanahangaika lakini mtu kwa kutumia social media amelala na mke wake na kiyoyozi anachallenge kazi zote za polisi anafundisha kazi zote za polisi mimi nikwambie ukiamua kujenga uadui na majeshi yetu hutakuwa salama sababu tutajua kuna mtu anakutuma wewe hauna thamani kuliko nchi yetu ya tanzania.
Watu wachache wasije wakatumiwa na watu wengine wa nje wakifikiri kwamba wanaweza kuondoa usalama wa nchi yetu amemalizia Sirro.
Sirro amesema hayo leo pindi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mara baada ya sakata la kupatikana kwa mfanyabaishara mkubwa nchini Mohammed Dewji aliyetekwa mnamo Oktoba 11 katika hoteli ya Collosseum na kupatikana alfajiri ya leo katika viwanja vya Gymkhana.
.