Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amewataka wanasiasa waliokimbilia nje ya nchi kwa madai ya kutishiwa usalama wa maisha yao kurejea Tanzania kwa kuwa kuna amani na yuko tayari kuwapa ulinzi.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Novemba 19, 2020, jijini Dar es Salaam, Sirro amesema mara baada ya kusikia aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA Tundu Lissu, anatishiwa maisha na hatimaye kukimbilia ubalozini, alikiandikia barua chama chake kwamba afike polisi kwa ajili ya kueleza undani wa nani anayemtishia lakini hakutoa taarifa.

Kamanda Sirro amesema kuwa watu wanaolalamika kuwa wanatishiwa huenda ukawa ni mpango mkakati wao wa kutafuta kuishi kwani kila mmoja anazo mbinu za kutafuta maisha.

” Hivi ukitishiwa kwa maneno, hata silaha jibu lake ni kukimbilia ubalozi?, hata mimi nimeshatishiwa kwamba Kamanda Sirro leo tutakushughulikia sasa nakimbia kwenda ubalozi gani, inategemea na mipango mikakati yake,”amesema IGP Sirro.

“Lema kwenye uchaguzi tumezungumza sana, lakini yeye anatishiwa kuuawa hakuna taarifa iliyotolewa polisi huo ni mchakato wa kutuchafua,” amesisitiza IGP Sirro.

Bofya hapa …………….

Simon Patrick aeleza kilichomuondoa Young Africans
VPL: Biashara United ugenini Dodoma