Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamini Mkapa – BMH, Dkt. Alphonce Chandika amewatoa hofu Watanzania juu ya chapisho lililotolewa hivi karibuni kuhusu kuvunjika kwa uume kwa baadhi ya staili wakati wa tendo la ndoa akisema wao walitoa tahadhari.
Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Jijini Dodoma, amesema wao wametoa taadhari kwa Watanzania hivyo wasiwe na uwoga juu ya jambo hilo kwani jambo hilo ni la uhuru na hawawezi kuwapangia watu.
Amesema, “tumetoa tahadhari tu kwa Watanzania na wala hatuwazuii huo ni uhuru wenu wenyewe kwa mtindo ambao unafurahia na mwenza wako, hatuna vizuizi lazima tuwe na mipaka kwa Wananchi ni wao tu kuamua uchukue tahadhari au huendelee kivyako ila sisi tumeshawapa taadhari.”
Hata hivyo, Dkt. Chandika ameongeza kuwa, “suala hilo la kuvunjika kwa uume limeibuka baada ya Mgonjwa mmoja kuja Hospitali kupatiwa matibabu baada ya kuathirika na mtindo huo na alipatiwa matibabu na ndio maana tukagundua tatizo hilo lipo, tukaamua kutoa taadhari kwa Wananchi.”