Baada ya timu sita (6) kutinga hatua ya Sita Bora ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirilkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufahamika, ratiba rasmi ya michuano hiyo, imetoka na inaonyesha kuwa hatua hiyo ya kutafuta bingwa wa msimu, itaanza Februari 18, mwaka huu.

Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine utaanza saa 10.00 jioni.

Ratiba inaonesha kwamba siku ya Februari 18, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na Sisterz.

Februari 20, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Panama saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi na Fair Play.

Februari 22, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisterz na Marsh Academy saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na JKT Queens.

Februari 24, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na JKT Queens saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Mlandizi Queens.

Februari 26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Sisters saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Marsh Academy.

Februari 28, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisters na Mlandizi Queens saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Fair Play.

Machi 2, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Acedemy na Fair Play saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi na Panama.

Machi 3, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu saa 10.00 jioni ambako JKT Queens watamaliza na Sisterz.

 

Pongezi Lipuli Kupanda Daraja
Pep Guardiola: Tunasubiri Majibu Ya Vipimo