Saa chache kabla ya kuikabili Biashara United Mara katika mchezo wa Mzunguuko wa 16 wa Ligi Kuu, Meneja wa Habari na Mawasilino wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Ahmed Ally ametoa orodha ya wachezaji ambao wataukosa mchezo huo.

Simba SC itakua mwenyeji wa Biashara United Mara, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, kuanzia saa moja Usiku leo Ijumaa (Machi 04).

Ahmed Ally ametoa orodha ya wachezaji wa Simba SC watakaoukosa mchezo huo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii (Instagram na Facebook).

Ahmed Ameandika: Katika mchezo wa leo tutawakosa wachezaji sita kutokana na kuwa majeruhi. Nyota hao ni Aishi Manula, Chris Mugalu, Kibu Denis, Hassan Dilunga, Jonas Mkude na Sadio Kanoute.

NOTE: MUGALU na KIBU ambao walikuwa nje ya uwanja kwa muda, tayari wameanza mazoezi, na utimamu wao wa mwili ukiwa sawa wataanza kushuka dimbani.

Simba SC inashika nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 31, huku wapinzani wao katika mchezo wa leo wako nafasi ya 13 kwa kumiliki alama 15.

Geita Gold wakanusha kuuza MECHI
Young Africans yaifuata Geita Gold Mwanza