Watu 6 wafariki dunia katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo Jijini Dodoma katika eneo la Kisasa ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Coaster na Lori.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Dodoma Dkt Ernest Ibenzi amethibitisha kupokea miili ya watu 6 ambao wamefariki dunia.
Dkt Ernest amesema majira ya saa 5 usiku usiku wa Disemba 29 wamepokea miili ya watu 16 huku 6 kati yao wakiwa wakiwa wameshafariki tayari.
“Ni kweli kuna ajali imetokea usiku wa kuamkia leo, ikihusisha Lori na Coaster na Hospitali ya Mkoa tulipokea miili ya watu 16, na kati yao 6 wakiwa wamekufa tayari, lakini pia bado hatujaitambua.” amesema Dkt Ernest.
“Hivi karibuni tutawapa taarifa zaidi kuhusiana na majina ya marehemu” ameongeza Dkt. Ernesti