Watu sita wameuawa wakiwemo watatu waliohusika katika shambulio hilo lililotokea majira ya asubuhi katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Msemaji wa polisi Fred Enanga amesema taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa wahusika wa mashambulio hayo ni wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF).
Alisema mshambuliaji wa nne alifuatwa na kuwekwa kizuizini na polisi walipata koti lenye bomu la kujitoa mhanga nyumbani kwake.
Bw Enanga aliongeza kuwa watu 33 walijeruhiwa na watano kati yao wako katika hali mbaya. ADF ilidai kuhusika na moja ya milipuko miwili mjini Kampala mwezi uliopita.
Mashambulio hayo mawili yalifanyika katika tofauti ya dakika 3 asubuhi ya leo katika kituo cha polisi cha kukagua magari karibu na kituo cha polisi cha central na mwengine ukatokea katika barabara ya bunge inayopita karibu na bunge la taifa hilo.