Rais wa Kenya, William Ruto amesisitiza kuwa Serikali yake haitolegeza kamba katika vita dhidi ya watu na makampuni yanayokwepa kulipa kodi, kauli ambayo hata hivyo imetafsiriwa kuwa inawalenga wapinzani wake.

Kwa majuma kadhaa sasa, rais Ruto, amekuwa akirushiana maneno kuhusu kodi na wapinzani wake, akidai suala la ulipaji kodi halitaangalia hadhi au nafasi ya mtu aliyonayo kwa jamii.

Rais wa Kenya, William Ruto. Picha ya The Standard.

Amesema, “Na mimi nimefurahi sana kwamba sasa Kenya yote tumeunganisha mawazo yetu na tumekubaliana hakuna mkubwa wala mdogo mbele ya sheria na sisi wote tutalipa ushuru kulinagana na mapato yetu.”

Katika hatua nyingine, Kiongozi wa upinzani nchini humo, Raila Odinga amemkosoa Ruto kwa kile alichosema anajificha nyuma ya suala la ulipaji kodi, ili kuficha ulegevu wa utendaji wa Serikali yake.

Waliokutwa na VVU JKT wapewa huduma maalum
Changamoto za ugumba nchini kupungua: Dkt. Mwinyi