Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa kasi ya ukuaji wa sekta ya madini imeongezeka kutoka asilimia 4 mwaka 2015 mpaka asilimia 4.8 mwaka 2018 baada ya marekebisho ya baadhi ya sheria na usimamizi bora katika sekta hiyo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Sekta ya Madini uliokutanisha wadau, wachimbaji wadogo wadogo wa madini, wafanyabiashara wa madini pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Madini uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema kuwa ili kuimarisha sekta hiyo hatosita kuwachukulia hatua Mawaziri na watendaji wa wizara hiyo pindi wanapokiuka utaratibu.

“Mimi ni ‘referee’ kazi yangu ni kadi ya njano na nyekundu, ya njano ni kuhamishwa Wizara na kadi nyekundu ni nje kabisa utabaki unautazama mpira,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Serikali imeweza kukusanya na kuvuka malengo ya ukusanyaji mapato ya shilingi bilioni 194 badala yake kuweza kukusanya shilingi bilioni 301 katika sekta ya madini ikiwa ni ongezeko la asilimia 53, na katika nusu ya mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali ilipanga kukusanya shilingi bilioni 160 lakini iliweza kuvuka malengo kwa kupata shilingi bilioni 167.54 sawa na asilimia 8 ya makusanyo.

 

Rais Magufuli aombwa kufuta leseni za kibiashara vyombo vya habari vya dini
LIVE IKULU: Rais Magufuli akizungumza na Viongozi wa Dini