Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa hategemei kuona vitendo vya rushwa vikitawala katika chaguzi zijazo, kwa kile alichokieleza ni juhudi kubwa zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika kutokomeza rushwa nchini.

Ameyasema mkoani Kilimanjaro wakati wa Kongamano la kumpongeza Rais Magufuli lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania UWT, ambapo aliwakilishwa na Naibu Spika, Tulia Ackson

“Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2015-2020, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekeleza Rais ni kurejesha nidhamu kwa watumishi, na kwa kazi kubwa aliyoifanya hatutaona rushwa kwenye chaguzi zijazo.”amesema Ndugai

Aidha, Naibu Spika amesema kuwa lingine ni kushughulikia tatizo sugu la rushwa ndani ya Serikali, na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hali ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa rushwa ya uchaguzi katika chaguzi zijazo.

Lissu ashinda pingamizi dhidi ya serikali
Hatuwatishi, bali ni ukweli- Kangi Lugola